Tuesday, September 29, 2009

Monday, September 28, 2009

Family Tears

Richard (Charles) akipokea majibu ya mama yake toka kwa doctor kuwa kutokana na sindano ya sumu aliyopigwa hatoweza kupona tena.
Charles Magali (Mr. Gondwe) na mkewe Farida Sabu (Mama Charles) wakigombana kuonyesha hawakuafikiana katika mambo fulani yahusuyo familia.

Mr. Daruweshi akimzuia Braiton (Kanumba) kuingia kwenye nyumba ambayo tayari ameshainunua katika moja ya scene za filamu ya Family tears


Farida Sabu (Mama Charles) katika moja ya scene aliyeshiriki kwenye filamu ya family tears akichomwa sindano na mmoja wa majambazi.

Wednesday, September 9, 2009

Red Valentine

Stella Bactazary aliyecheza kama Dada yake Jacqueline Wolper (Victoria) katika moja ya scene ya filamu ya Red Valentine. Stella Bactazary anamsema Jacqueline Wolper (Victoria) kwa kuzaa mtoto wa kizungu na kutia aibu familia.

Wema Sepetu na Steven Kanumba waliyocheza kama mke na mme katika moja ya scene ya Red Valentine

A. Steven Kanumba (Nicholaus) na Jacqueline Wolper (Victoria) waliocheza kama mtu na mpenzi wake katika moja ya scene ya filamu ya Red Valentine

Wema Sepetu (Vivian) anamuomba Steven Kanumba (Nicholaus) wakae waongee ili wayamalize na waweze kupatana katika baadhi ya scene ya filamu ya Red Valentine.

Baadhi ya scene ya filamu ya Red Valentine anaonekana Steven Kanumba (Nicholaus) anarudi nyumbani baada ya siku tatu, Wema Sepetu (Vivian) anamuuliza alikokuwa.

A. Wema Sepetu (Vivian) akimshukuru Mungu baada ya kuambiwa ni mjamzito katika moja ya scene ya filamu ya Red Valentine

Doctor anawaelezea Steven Kanumba (Nicholaus) na Wema Sepetu (Vivian) waliocheza kama mme na mke katika moja ya scene ya Filamu ya Red Valentine sababu za mwanamke kutokushika mimba au sababu za mwanaume kukosa uwezo wa kumpa mwanamke mimba.

Fake Smile

A. Aunty Ezekiel (Bethel) anampa kikapu cha mboga dada yake Neshi Adam (Batuli) ili aende akapike katika moja ya scene ya filamu ya Fake Smile.

A. Steven Kanumba (Jonson) na Richard Oyle Bezuidenhout (Dikson) katika moja ya scene za filamu ya Fake Smile, Kanumba anamwambia Richard waachane na mpenzi wake Neshi Adam (Batuli)
Tania na Richard Oyle Bezuidenhout (Dickson) waliocheza kama mtu na mpenzi wake katika moja ya scene za filamu ya Fake Smile, Tania akifurahia pesa alizoingia nazo Richard Oyle Bezuidenhout (Dickson) baada ya kupewa na Neshi Adam (Batuli) ambaye pia ni mpenzi wa Richard (Dickson)

Richard Oyle Bezuidenhout (Dickson) anamuomba msamaha Neshi Adam (Batuli) kwa kumgonga na baiskeli na kumuangushia vitabu vyake katika moja ya scene za filamu ya Fake Smile
Neshi Adam (Batuli) anampatia funguo za gari yake Richard Oyle Bezuidenhout(Dickson) waliocheza kama mtu na mpenzi wake katika moja ya scene za filamu ya Fake Smile

A. Claudi (Kibosile) katika moja ya scene za Fake Smile anampa
Aunty Fifii hela ili aweze kuondoka na Neshi Adam (Batuli) kwenda kufanya nae mapenzi.

A. Katika moja ya scene za filamu ya Fake Smile, Hamisi Abdallah (Muba) kamleta Neshi Adam (Batuli) kwa Aunty Fifii ili afanye kazi.

Neshi Adam (Batuli) anambembeleza mama yake baada ya baba yake Aunty Ezekiel (Bethel) kumtolea maneno ya kashfa katika moja ya scene za filamu ya Fake Smile

Neshi Adam (Batuli) anafurahia kwa kitendo cha mdogo wake Aunty Ezekiel (Bethel) kurudi nyumbani katika moja ya scene ya filamu ya Fake Smile

Steven Kanumba (Jonson) anamwambia Richard Oyle Bezuidenhout (Dickson) aeleze ukweli kuhusu uhusiano wake yeye na Neshi Adam (Batuli) katika moja ya scene ya filamu ya Fake Smile.

Aunty Ezekiel (Bethel) akimkebehi dada yake Neshi Adam (Batuli) waliocheza kama mtu na dada yake katika moja ya scene ya filamu ya Fake Smile

Back Home